Mnamo tarehe 5 na 6 Februari 2019 chini ya ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNAIDS Ofisi ya NACOPHA Kanda ya Mwanza ilifanya ziara
ya kimafunzo ya kubadilishana uzoefu juu ya utekeleaji wa shughuli za mwitikio wa UKIMWI ili kuhakikisha kuwa 90% 90% 90% zinafikiwa ifikapo 2030. ( ambapo 90% ya kwanza ni kwa waliopima afya zao watambue hali zao za maambukizi, 90% ya pili ni wanaostahili kupatiwatiba wanapata tiba na kubakia katika tiba na
90% ya waliopo kwenye tiba wawe na kiwango kidogo cha Virusi kwenye damu
Katika
ziara hiyo Konga za Halmashauri ya Igunga na Biharamuro walikuwa wageni
walioitembelea konga ya Muleba. Konga hizo ziliwakilishwa na Wenyeviti wa
Konga, Waratibu wa kudhibiti UKIMWI Halmashauri (CHAC ), Mwenyekiti
wa kamati ya kuzibiti UKIMWI Halmashauri (CMAC), Mwenyekiti wa kamati za
kudhibiti UKIMWI ngazi ya kata (WMAC) na
viongozi wawili wa Vikundi wezeshi.
Wageni hao toka Igunga
na Biharamuro walitembelea na kuona miradi mbalimbali inayotekelezwa na vikundi
vya wezeshi vya WAVIU vya Tumaini kutoka Kishanda, Imani kutoka Bunganhuzi na
Njuna ya June kutoka Mushabago,
Wanakikundi wa kikundi cha Imani wakionesha moja ya miradi yao ya ufugaji wa mbuzi |
pia walitembelea Vituo vya Tiba na matunzo (CTC - Care and Treatment Center) vilivyopo Buganguzi na kituo cha Afya cha Rushwa.
Wageni wakipata maelezo kutoka kwa Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Buganguzi |
Viongozi wa Biharamuro, Igunga na Muleba walipendezewa na ziara hiyo ya
mafunzo na kubadilishana uzoefu na kupendekeza
kufanyika mara kwa mara. Pia walitoa uzoefu wao kama mapendekezo kwa konga ya
Muleba na Vikundi Wezeshi vya Konga hiyo.
Pamoja na mapendekezo
hayo waliyoyatoa waliwashukuru na kuwasifu Konga na Vikundi Wezeshi vya WAVIU wa
Muleba kwa vitu vifuatavyo:-
•
Kuratibu
na Kusaidia Vikundi vya Wezeshi vinavyoundwa na halmashauri ya Muleba
·
Huduma
za ART zinazotolewa katika ngazi ya kituo
Huduma,
Ushirikiano na utetezi kwa WAVIU unaotolewa katika zahanati/CTC ya Rushwa na
Buganguzi
•
WAVIU
wengi wa Konga Muleba Virusi vyao vimefubaa kitu kinachowawezesha kujikita
zaidi kwenye shughuli za maendeleo ya kiuchumi na Kijamii
•
Msaada
unaotolewa na vikundi vya Wezeshi katika
kuwalea watoto yatima wanaoishi na VVU
na wasiokuwa na VVU
Watoto wanaolelewa na kusomeshwa na wanakikundi wa kikundi cha Imani baada ya wazazi wao kufariki |
Tushebe Matunda ni mtoto wa miaka minne (4) anaelelewa na wanakikundi wa Tumaini Kishanga baada ya Mzazi wake kufariki siku sita kabla ya kujifungua |
Baada ya ziara hii kulifanyika kikao cha majumuisho kwa konga zilizoshiriki Igunga, Muleba na Biharamulo kwa kuangalia nini wamejifunza ,nini wanashauri kifanyiwe kazi na kukubaliana ni kipi wanakwenda kufanyia kazi ambapo moja ya ahadi zilizotolewa ilikuwa ya mwenyekiti wa Halmashauri ya Igunga bwana Lucas Bugota aliyeahidi kuwa " mimi pamoja na viongizi wa Konga tuliokuja kujifunza tukitoka hapa tutaenda kuandaa mpango kazi kwa ajili ya utekelezaji wa yale yote tuliojifunza tunaomba baada ya miezi mitatu mje igunga kwa ajili ya kuona shughuli zetu tulizozifanyia maboresho na kujifunza pia"
Mnamo 7 Februari 2019, NACOPHA ilitoa mrejesho/ mapendekezo kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya ya Muleba, aliyefurahia na kupendezwa na kazi kubwa inayofanywa
na Konga ya WAVIU wa Halmashauri ya
Wilaya ya Muleba.
Kikao cha mrejesho wa ziara na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba Mhe. Emanuel Sherembi |
Mapendekezo yaliyotolewa ni pamoja
na Halmashauri zione jinsi gani zitawatumia WAVIU/ Wakili tiba kusaidia kutoa
huduma ambazo sio za kitabibu katika vituo vya afya ili kupunguza adha ya
upatikanaji wa huduma katika vituo vya tiba na matunzo, Mashirika yanayofanya miradi
ya afua za UKIMWI kutumia mfumo rasmi wa konga kufanya kazi na WAVIU tofauti na
ilivyo sasa wanawatumia WAVIU bila kupita Konga ,Viongozi wa dini wapewe
mafunzo juu ya masuala ya VVU/UKIMWI kwa sababu wengi wao wamekuwa
wakiwashawishi WAVIU waache dawa mara baada ya kuombewa.
Post a Comment