Na Friday Simbaya,
IRINGA
Mkuu wa
Wilaya ya Iringa Richard Kasesela,
amewataka wanaume kujitokeza kwa wingi kupima VVU ili kujua hali zao na kama
wakugundulika waanze dawa mara moja.
Alisema kuwa
utafiti unaonesha kwamba wanaume wako nyuma katika masuala ya kupima VVU
ukilinganisha na wanawake.
Kasesela
alisema hayo wiki iliyopita wakati wa uzinduzi wa filamu itwayo ‘PILI’ ya
masuala ya VVU na UKIMWI katika Mkoa wa Iringa katika viwanja vya Mwembetogwa,
iliyoanza kuonekana kuanzia saa moja 1 jioni hadi saa tatu usiku.
Alisema kuwa
Iringa inakabiliwa na changamoto ya masuala ya UKIMWI kwa vile inashika nafasi
ya pili katika maambukizi ya VVU baada ya Mkoa wa Njombe anaoshika nafasi ya
kwanza kitaifa.
Kasesela
alieleza kuwa kuna faida ya kupima VVU
na hatimaye kujua hali yako kwa vile Serikali inatoa ARVs za kupunguza makali
ya VVU bure kupitia Msaada wa Mfuko wa dharura wa Raisi wa Marekani wa
kupambana na UKIMWI (PEPFAR).
“Kupima VVU
na kujua hali zetu za afya hasa kwa wanaume kutapunguza kasi ya maambukizi ya
VVU mkoani Iringa, hivyo naomba wanaume wenzangu tuwe mstari wa mbele”
Alihimiza DC Kasesela.
Pia
alilipongeza Baraza la Taifa la Watu Wanaishi na VVU (NACOPHA) kwa kushirikiana
na Ubalozi wa Marekani kwa onesho la filamu ya “PILI”.
Inalenga
kuwafikishia ujumbe vijanakukiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya miaka 15 ya
msaada wa PEPFAR katika kuwezesha wanaoishi na VVU (WAVIU) hasa vijana.
Mratibu wa uzinduzi wa filamu ya “PILI” kutoka
NACOPHA bwana Edward Uisso alisema lengo kuu la onesho la filamu/sinema hii ni ukuza ongezeko
na ufikiwaji wa huduma za VVU hususani kwenye tiba na matunzo miongoni mwa
vijana wadogo wanaoishi na VVU kupitia kutambua mchango na msaada wa PEPFAR
katika mwitikio wa kitaifa wa UKIMWI kwa kutumia WAVIU kama wanufaikaji wa
msaada kutoka PEPFAR nchini Tanzania.
Aliongeza
kuwa malengo mengine ni kushirikisha jamii katika ongezeko la ufikiwaji na
utumiaji wa huduma za VVU hasa kwenye tiba na matunzo na kutumia filamu hii
kama zana ya uwezeshi kwa vijana wadogo
wanaoishi na VVU katika kutatua na kupambana dhidi ya unyanyapaa na ubaguzi.
Uisso
aliongeza kuwa unyanyapaa binafsi kwa WAVIU bado ni changamoto kubwa ukiachilia
mbali unyanyapaa utokanao na tamaduni na imani za kidini.
Alisema
ushirikishwaji wa jamii ni ufunguo katika kuelimisha jamii juu ya madhara ya
unyanyapaa kwa WAVIU na katika kufikia sifuri ya unyanyapaa ifikapo mwaka 2030.
“Uzinduzi
huu wa filamu ya PILI ni wa tano kimkoa,
kwani kwa mara ya kwanza filamu hii ilizinduliwa kwa mkoa wa DSM tarehe
8/11/2018, Mwanza tarehe 23/11/2018, Mbeya tarehe 30/11/2018, Njombe ni leo
tarehe 7/12/2018 na kilele kitakuwa kwa Mkoa wa Iringa tarehe 14/12/2018 ikiwa
ni kubadilishana uzoefu kwa watu wanaoishi na VVU kama wanufaikiaji wa msaada
wa PEPFAR nchini”. Alisema Uisso.
PILI
anaishi kijijini nchini Tanzania,
akifanya kazi ya kibarura shambani akilipwa ujira wa chini ya dola mbili (Sh
2,600) kwa siku ili aweze kupata chakula kwa watoto wake wawili
Anaishi
anahangahika kukabiliana na hali yake ya kuwa na VVU kwa kificho.
Post a Comment