Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro
Rodriguez alipowasili katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma katika hafla ya
maadhimisho ya Siku ya ukimwi duniani leo tarehe 01 Desemba 2018. Kushoto ni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenyeulemavu.
Waziri Mkuu wa
Tanzania, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma,
Profesa Davis Mwamfupe alipowasili katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma
katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya ukimwi duniani leo tarehe 01 Desemba
2018. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustine Kamuzora.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akikagua baadhi ya
mabanda yaliyokuwa yakionyesha shughuli mbalmbali zinazoendeshwa na wadau
alipotembelea mabanda hayo wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya ukimwi
duniani leo tarehe 01 Desemba 2018 jijini Dodoma..
Baadhi ya
waandamanaji toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora
wakipita katiika maandamano wakati wa hafla ya siku ya ukimwi duniani leo
tarehe 01 Desemba 2018 jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa hafla
ya maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani leo tarehe 01, Desemba 2018 jijini
Dodoma. Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,
Ajira, Vijana na Wenyeulemavu Mhe. Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu Mhe. Jenista
Mhagama akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani leo
tarehe 01, Desemba 2018 jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
Binilith Mahenge, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko.
Mkurugenzi Mkuu
wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko akizungumza wakati
wa hafla ya maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani leo tarehe 01, Desemba 2018
jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu Mhe.
Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na
Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile.
Mwenyekiti wa
Baraza la Watu Wanaosihi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOPHA), Bi. Leticia Mourice
akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani leo tarehe
01, Desemba 2018 jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim
Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na
Wenyeulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya
Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko.
Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2018/19 - 2022/23 leo tarehe
01 Desmba 2018 jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu Mhe.
Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Mussa Sima. Mkakati huo unatarajia kupunguza
maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 85
ifikapo mwaka 2023.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI,
Seleman Jaffo nakala ya Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2018/19 - 2022/23
leo tarehe 01 Desmba 2018 jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais Mazingira na Muungano, Mussa Sima na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus
Nyongo. Mkakati huo unatarajia kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75
ifikapo mwaka 2020 na asilimia 85 ifikapo mwaka 2023.
Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
nchini, Alvaro Rodriguez nakala ya Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI
2018/19 - 2022/23 leo tarehe 01 Desmba 2018 jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Muwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia UKIMWI Duniani
(UNAIDS) Dkt. Leo Zekeng, Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile. Mkakati
huo unatarajia kupunguza
maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 85
ifikapo mwaka 2023.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya wadau wa masuala ya Ukimwi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani
iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma leo. (Picha zote na: Frank Shija - MAELEZO,
Dodoma)
Post a Comment