Mkutano Mkuu wa tatu wa Baraza la
Taifa la Watu wanaoishi na VVU ulianza mnamo tarehe 15 Novemba 2018
nakumalizika tarehe 16 Novemba 2018, katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini
Dodoma.
Mkutano huo ulifunguliwa na katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, ajira, vijana, na watu wenye ulemavu Prof.
Faustin Kamuzora aliyemuwakilisha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.
Serikali imewaahidi watu
wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI nchini kutofumbia macho changamoto
wanazokabiliana nazo na kuhakikisha inaendelea kuboresha huduma za UKIMWI hapa
nchini hayo yalisemwa kupitia hotuba ya
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa iliyosomwa kwa niaba yake na Prof. Faustin
Kamuzora
Amesema kupitia hotuba ya
mwenyekiti wa NACOPHA bwana justine Mwinuka alibaini changamoto mbalimbali
zinazowakabili WAVIU ambazo ni pamoja na umbali wa vituo vya matibabu na
kutumia muda mrefu kwenye vituo vya matibabu,kipato duni cha WAVIU kugharamia
matibabu,lugha na vitendo vya unyanyapaa katika vituo vya kutolea huduma, uhaba
wa mashine za kupimia wingi wa Virusi kwenye damu na kuratibu wadau wote kwa Ushirikishwaji
wa WAVIU kwenye mwitikio wa UKIMWI kupitia muundo wa konga za WAVIU.
Aidha amesema katika kukabiliana
na changamoto hizi, serikali imeendelea kufanya juhudi za kuzipunguza na hata
kuzimaliza kabisa kwa kuongeza idadi ya vituo vya afya vinavyotoa huduma ya matibabu ya VVU “hadi
kufikia July 2018 tuna vituo visivyopungua 8000 vya kutolea huduma za matibabu
ya VVU, pia tumeweza kusajiri WAVIU 839,544 kufikia mwishoni mwa mwaka 2017”
Mkutano huu umeenda sambamba na Baraza
kutambua na kutunukia nishani za heshima kwa baadhi ya Viongozi kwa kutambua
michango yao mikubwa katika mwitikio wa UKIMWI.
Waliotunukiwa nishani hizo ni
pamoja na Mhe, Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim
Majaliwa, Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai,
Mkurugenzi
mstaafu wa TACAIDS Bi. Fatuma Mrisho, Mwenyekiti mstaafu wa NACOPHA bwana
Vitalis Makayula na Mwenyekiti wa NYP+ Nevala Kyando.
Pamoja na hayo Mkutano Mkuu
uliweza kuwachagua viongozi Bodi ya Baraza la Taifa la WAVIU ambapo wafuatao
walichaguliwa kuwa viongozi wa bodi kwa nafasi ya Mwenyekiti ilitwaliwa na Bi Leticia
Mourice Kapela wa konga ya Bukombe, Makamu Mwenyekiti bwana Yusufu Alfred Merere
mweka hazina Mitterrand Mohamed Dagila na wajumbe Shamila Ibrahim, Elias Charles, Christina
Martin, Deogratius Clevass, Francis Stolla, Hermes Mutagwaba, Pudensiana
Mbwiliza na Amir Mahamud.
Mbali na uchaguzi wa bodi
walichaguliwa pia wawakilishi wa WAVIU kwenye TNCM ambao ni Japhes Baitani na Pudensiana
Mbwiliza
Mkutano mkuu wa NACOPHA hufanyika
kila baada ya miaka mitatu kwa kuwakutanisha wawakilishi kutoka Tanzania Bara
na wadau wengine wa UKIMWI ukiwa na lengo la kutathimini utekelezaji wa Baraza
kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kupata taarifa ya mwelekeo wa Baraza
kwa kipindi kinachofuata na kujadiliana kuhusu mafanikio na changamoto
zinazowapata WAVIU kote nchini pamoja na
utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa
kufikia tisini tatu (90-90-90) .
Post a Comment