Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,  Kazi, ajira, vijana, na watu wenye ulemavu Prof. Faustin Kamuzora amesema Tanzania inakadiriwa
 kuwa na watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI 1,400,000 ambapo nusu ya hao hawajitambui kuwa wanaishi na VVU.


Prof. Kamuzora aliyasema hayo leo Jijini Dodoma alipokua akifungua Mkutano Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA) kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Amesema kuwa Serikali ya Tanzania imefanya juhudi kubwa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo na hasa wanaume na vijana, kujitokeza kupima afya zao na kujua hali zao za maambukizi.
“Nachukua fulsa hii kuwapongeza kipekee kabisa wanachama wa NACOPHA kwa ujasiri wao wakuweza kupima nawale waliokutwa na maambukizi ya VVU kuweza kujitokeza kupata huduma mbalimbali za matibabu”. Alisema Prof. Kamuzora na kuongeza kuwa.
“Hongera nyingi nizitoe kwa jitihada kubwa sana mlizofanya kuweza kupima nakuanza tiba ukizingatia hapo awali suala la kuanza tiba halikufanyika sambamba na kupima kama iliyo hivi sasa, “alisema.
Aidha aliwataka Watanzania kujiwekea utaratibu wa kupima afya zao ili kujua hali zao na endapo wakigundulika wanamaambukizi waanze tiba mapema  kwani kwa sasa mazingira ni rafiki na dawa zinapatikana bure katika vituo vyote vya afya.
Prof. Kamuzora alisema serikali kamwe haitafumbia macho changamoto mbalimbali zinawapata watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI na badala yake Serikali inaendelea kufanya juhudi za kupunguza  kumaliza kabisa changamoto hizo.
Amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto hiyo Serikali imeongeza idadi ya vituo vya afya vinavyotoa huduma ya matibabu ya VVU ambapo hadi Julia 2018 kulikuwa na vituo 8000 vya kutolea huduma ya matibabu.
“Pia tumeweza kusajili watu wanaoishi navirusi vya ukimwi 839,5 kufiki mwishon mwa mwaka 2017 ambayo inajumisha watu wazima na watoto” alisema.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi bara Justin Mwinuka aliasema wanakabiliwa na changamoto ya umbali wa vituo vya matibabu na kupelekea kutumia muda mrefu kwenye vituo vya matibabu  hali inayochangia utoro wa kupata huduma hiyo.
Amesema lugha na vitendo vya unyanyapaaji kutoka kwa watoa huduma kwenye vituo vya afya ni kubwa hali inayowafanya watu wengi na hasa wajawazito, vijana, wasichana, na wenye umri balehe wasiende kupata katika vituo hivyo
Habari na Fullshangwe Blog