Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na
VVU Tanzania (NACOPHA) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani wazindua filamu ya Vijana
kuhusu VVU na UKIMWI iitwayo ‘PILI” tarehe 8/11/2018 katika Ukumbi wa sinema
Mlimani City, jijini Dar es salaam.
Filamu hii ni ya kwanza na yenye
visa halisia vya kijamii inayoangazia maisha ya wanawake wanaoishi na VVU katika
Afrika Mashariki. Ni mojawapo ya filamu chache zilizotengenezwa barani Afrika
zinazohusisha wanawake ambao wengi wao si waigizaji.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huu
alikuwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Mohamed Bakari, ambapo pamoja na mambo mengine aliwahasa washiriki
hasa vijana kuwa mstari wa mbele katika mwitikio wa UKIMWI.
Aidha wakati wa uzinduzi huo Kaimu
Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk,Inmi Patterson amesema hii ni filamu
ya Kitanzania iliyotambuliwa na matamasha makubwa ya filamu duniani inayohusu
kuwatetea watu wanaoishi na VVU.
Akizungumzia filamu hiyo, Dk.Patterson
amesema filamu hii imetengenezwa na vijana wa Kitanzania ikiwa imebeba maudhui
ya kuwatetea watu wanaoishi na VVU Tanzania, ambapo waigizaji wake wengi
ni wale ambao hawajapitia mafunzo rasmi.
Amesema filamu hii imeoneshwa kwa mara ya kwanza Jijini London wiki
chache zilizopita ambapo Matamasha makubwa ya filamu yameitambua filamu hiyo.
“Kama sehemu ya maadhimisho ya miaka
15 ya Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI nchini Tanzania,
Ubalozi wa Marekani unashirikiana na Baraza la Taifa la Wanaoishi na VVU
(NACOPHA) kwa ajili ya kuendelea kuionesha filamu hii katika Mikoa mbalimbali
ambayo ni Mwanza,Mbeya,Njombe na Iringa,”amesema Dk.Patterson.
Pia Mkurungezi Mtendaji wa NACOPHA Ndugu Deogratius Rutatwa alihitimisha kwa
kusema lengo kuu la uzinduzi wa filamu hii kwa Jiji la Dar Es Salaam na Mikoa
iliyoteuliwa ni kukuza ongezeko na ufikiwaji wa huduma za VVU
hususani kwenye tiba na matunzo miongoni mwa vijana wadogo wanaoishi na VVU
kupitia kutambua mchango na msaada wa PEPFAR katika mwitikio wa Kitaifa wa
UKIMWI kwa kutumia WAVIU kama wanufaikaji wa msaada kutoka PEPFAR nchini
Tanzania.
Picha Mbalimbali za matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati wa uzinduzi wa filamu ya PILI
Good this important filam , Thanks USAID funds thanks Nacophatz staff and all's Members of Board for nacophatz ,this Good jobs , Thanks Tanzania Government coraborating in general , Thanks God
ReplyDelete