NACOPHA Kanda ya Mwanza imefanya Mkutano wa kutathmini mwenendo wa mradi wa SAUTI YETU
unaotekelezwa na NACOPHA kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa
la Marekani
(USAID),
katika Halmashauri nane za Mikoa ya Kanda ya Mwanza . Mkutano huu umefanyika
tarehe 05/07/2018 Monarch hotel Jijini Mwanza.
Mkutano huo ulihudhuliwa na wenyeviti na Makatibu wa Konga, pamoja na Waratibu wa Kuthibiti UKIMWI Halmashauri ( CHAC na DAC) kutoka katika wilaya za Nyamagana, Ilemela, Sengerema, Muleba, Musoma, Nzega Igunga na Kahama mji.
Mkutano huo ulifunguliwa na Mratibu wa UKIMWI mkoa wa Mwanza, lakini pia Ulihudhuriwa na Mratibu wa Kuthibiti UKIMWI TACAIDS Mkoa wa Mwanza, Mwenyekiti wa Baraza na baadhi ya wajumbe wa Bodi, Afisa mtendaji mkuu na watendaji wa Baraza.
Lengo la Mkutano huo lilikuwa ni kutathmini mwenendo wa
utekelezaji wa Mradi wa SAUTI YETU, mafanikio na Changamoto zinazopatikana
katika kipindi cha utekelezaji cha mradi, lakini pia kujadili kwa pamoja namna ya
kutatua changamoto hizo kwa pamoja ili kufikia malengo yaliyoadhimiwa na Mradi
wa SAUTI YETU.
Post a Comment