Konga ya Baraza la Taifa la Watu waishio na Virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA)
halmashauri ya wilaya ya Kinondoni imefanya
uchaguzi wa viongozi wa konga hiyo mapema tarehe 23 /2/2019 katika ukumbi wa
halmashauri ya wilaya ya kinondoni.
Uchaguzi ulifanyika kwa ufadhili wa watu wa Marekani (USAID) Kupitia
Mradi wa CHSSP unaotekelezwa na JSI, ambao moja ya malengo yake ni kuzijengea
uwezo Konga katika masuala ya uongozi bora.
Uchaguzi huo ulisimamiwa na
Viongozi kutoka halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, Mratibu wa NACOPHA Kanda ya
Dar es Salaam, wenyeviti wa kamati ya kudhibiti UKIMWI (CMACs), Mwakilishi wa mratibu
wa UKIMWI ngazi ya halmashauri (CHACs) Mwakilishi wa Mratibu wa UKIMWI wilaya upande wa tiba (DACC) pamoja na Mratibu wa Mradi wa CHSSP kutoka JSI.
Wageni waliohudhulia kushuhudia uchaguzi huo ni pamoja na baadhi ya
viongozi kutoka Konga jirani ambazo ni Temeke, Ilala, Kigamboni na Ubungo.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni pamoja
na:
Mwenyekiti - Juma Galaba.
makamu-nikokwisa Jeremiah.
Katibu-Suleiman Lweno.
Mwekahazina-Kisa Mbonile.
Viongozi wengine waliochaguliwa ni wajumbe wa Konga,
Uwakilishi wa Vijana, Me - Said hamis na Mansue Ramadhani. Ke- Shan Ally na Catherin Swai ,
Wawakilishi wa Wazee me- Mtume Mmakasa na Shahaban Bwanga. Ke ni Aisha kupanga
na Doto Sanga pamoja na wajumbe wawili watakao wakilisha katika kamati ya
kudhibiti UKIMWI ya Wilaya (CMAC) ambao ni Majuto Mwinyihija na Margret Sinda
Baraza kupitia
Afisa Mtendaji Mkuu inatoa pongezi kwa viongozi waliochaguliwa na kuwataka
watekeleze wajibu wao kufuatana na sheria ya baraza inavyowataka wafanye “Nawapongeza
Sana. Viongozi wote karibuni kwenye ofisi yenu tujuane tupange kazi kwa pamoja,
msihofu tuko tayari kwa uwajibikaji. Ahsante kwa uongozi uliopita kuwezesha hili
pamoja na JSI na ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa pamoja na CHAC. Ahsante Mratibu wa Kanda ya Dar es
Salaam kwa kutuwakilisha. Ahasante Viongozi wa Konga zingine kwa kuonyesha
mshikamano. Tushikamane sote kwa maslahi na ustawi wa WAVIU wote Tanzania”
shukrani za Afisa Mtendaji Mkuu.
Hivi sasa Baraza lina konga zipatazo
167. Baraza linatoa shukrani za dhati kwa JSI R&T
kupitia mradi wa CHSSP kwa kufanya kazi kwa Karibu na Baraza kwa kuhakikisha
malengo ya pamoja ya kufikia 90-90-90 yanafikiwa.
Post a Comment