Tarehe 1 Desemba ya kila mwaka
huwa ni siku ya UKIMWI duniani, Nchi mbalimbali huadhimisha siku hiyo kwa ajili
ya kuwakumbuka waliofariki kwa ugonjwa wa UKIMWI pamoja na kukumbushana
kuendeleza mapambano dhini ya ugonjwa huu hatari ambao hadi hivi sasa hakuna
tiba wala kinga iliyogundulika.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania Bw. Deogratius Rutatwa akizungumza katika kipindi cha KUMEKUCHA kinachorushwa na ITV Tanzania katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani Disemba 1, 2017
Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania Bw. Deogratius Rutatwa akizungumza katika kipindi cha KUMEKUCHA kinachorushwa na ITV Tanzania katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani Disemba 1, 2017
Wananchi wakiwa kwenye maandamano wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 |
Kwa mwaka huu wa 2017
maadhimisho haya kitaifa nchini Tanzania yalifanyika katika viwanja vya mnazi
mmoja jijini Dar es Salaam ambapo katika kilele cha maadhimisho hayo mgeni
rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia
Suluhu Hassan. Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “Changia
mfuko wa Udhamini wa UKIMWI okoa maisha”
maandamano wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 |
Pamoja na hayo katika siku hii,
watu wote hukumbushwa kipima na kuzilinda afya zao bila kusahau kuwajali wale
wanaoishi na maambukizo ya Virusi vya UKIMWI. Elimu madhubuti hutolewa jinsi ya
kuishi ukiwa tayari Una maambukizo ya VVU kwani ukigundulika kuwa unamaambukizo
ya VVU unatakiwa kuanza/ kuanzishiwa tiba mara moja na kusisitizwa kuto acha
kunywa dawa za ARV kwa ajili ya kuvubaza na kupunguza makali ya VVU ili
usifikie hatua ya UKIMWI ambayo ni hatari Zaidi.
Kuwa na Virusi vya UKIMWI siyo
mwisho wa maisha kwani mtu aishiye na maambukizo ya VVU kwa kutumia dawa za ARV
ataweza kuishi maisha marefu, kuwa na nguvu ambazo zitamsaidia kujikimu
kimaisha kwa kuendelea kujishughulisha kwani mwili unakuwa na nguvu hivyo mtu huweza
kuishi maisha marefu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU (NACOPHA) wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam |
Katika jamii zetu kumekuwa na
changamoto nyingi na mitazamo tofauti dhidi ya watu wanaoishi na VVU. Watu wanadhani kuwa ukiwa
karibu na mtu anaeishi na VVU basi na wewe utaweza kupata maambukizo hayo.
Elimu madhubuti bado inahitajika katika jamii zetu, ili kupinga unyanyapaa na
matendo maovu wanayofanyiwa watu wanaoishi na VVU.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU Tanzania Ndugu Justine Mwinuka Mwenye suti nyeusi akiwa na baadhi ya wajumbe wa Bodi Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa NACOPHA mwenye kofia katika Kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani Dec 1 2017 |
UKIMWI ni ugonjwa kama yalivyo
magonjwa mengine ya Kansa, Presha, Malaria, Kipindupindu, n.k ambayo
yasipotibiwa au kupewa angalizo la juu hupelekea kifo.
Wanachi walihudhulia na wakipima shinizo la Damu wakati wa maadhimisho hayo. |
UKIMWI husambazwa kwa damu ya
mtu mwenye Maambukizo kukutana na damu ya mtu asiyekuwa na maambukizo. Damu
hiyo huweza kukutana kipindi watu wanapofanya ngono bila kutumia kinga
(kondom), kushirikiana kutumia vifaa vyenye ncha kali na mtu mwenye VVU, mama
mwenye VVU kwenda kwa mtoto (kipindi cha kujifungua au kumnyonyesha mtoto), pamoja
na kuhamishiwa damu iliyokuwa na VVU. Hizo ndio njia kuu zinazoweza kusababisha
maambukizo ya VVU toka kwa mtu mwenye VVU kwenda kwa mwingine.
Mratibu kutoka Baraza la Taifa la WAVIU Tanzania (NACOPHA), Bi Edna Edson akimuelezea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan huduma wanazotoa za mapambano ya Ukimwi alipotembelea mabanda katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. |
Wananchi wakiwa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) alipotembelea banda hilo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. |
Post a Comment