Baraza la Taifa la Watu waishio
na Virusi vya UKIMWI Tanzania limefanya uchaguzi wa viongozi wa Konga mpya ya
Kigamboni mapema 18 /7/2017 katika ukumbi wa CCM uliopo katika kata ya
Kigamboni wilayani Kigamboni. Uchaguzi huo uliofanywa kwa ufadhili wa watu wa
Marekani (USAID) Kupitia Mradi wa CHSSP unaotekelezwa na JSI ambao moja ya
malengo yake ni kuzijengea uwezo Konga katika masuala ya uongozi bora.
Wanakonga wa kigamboni wapatao 31
walihudhulia na kufanikiwa kuwachagua viongozi wafuatao
1.
JOSHUA PIMA NYAGANGO - Mwenyekiti wa
Konga ya Kigamboni,
2.
MARIA YUSUF - Makamu Mwenyekiti,
3.
AISHA SAIDI BURE - Katibu
4.
MWANAHAMISI ISIAKA - Mtunza fedha (Mweka hazina) wa Konga ya
Kigamboni.
Pia wajumbe wa bodi ya Konga walichaguliwa ambapo:-
1.
SAUDA MIKIDADI amekuwa muwakilishi wa
vijana wa kike
2.
PAUL MICHAE NZIJE muwakilishi wa vijana
wa kiume.
3.
NICOLAUS SIKA na IBRAHIM ABDURABI MOHAMED wakiwakilisha
wajumbe wanaume
4.
HADIJA SHABANI pamoja na HIDAYA MOMBA
wakiwakilisha wajumbe wanawake.
Ndugu IBRAHIM ABDURABI
MOHAMED alichaguliwa kuwa muwakilishi wa Kamati ya UKIMWI ya halmashauri (CMAC)
na Katibu wake ni Bi AISHA SAIDI BURE.
Katika uchaguzi huo
wadau mbalimbali wa masuala ya VVU na UKIMWI walihudhuria, kulikuwa na
wanavikundi toka katoka vikundi vya WAVIU waliotokea katika kata 9 za kigamboni
wapatao 31, CHAC, DAC, Mwakilishi toka TACAIDS, Mwakilishi toka Halmashauri ya
wilaya ya Kigamboni, viongozi toka konga ya Temeke na Ilala ambao walikuwepo
kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo.
NACOPHA inatoa pongezi
kwa viongozi hao waliochaguliwa na kuwataka watekeleze wajibu wao kufuatana na
sheria ya baraza inavyowataka wafanye, pia inatowa shukrani kwa JSI kupitia
mradi wa CHSSP kwa kufanya kazi kwa Karibu na Baraza kwa kuhakikisha malengo ya
pamoja ya kufikia 90%,90%,90% yanafikiwa.
Bira kusahau Serikali kupitia kwa
viongozi wa wilaya, CHAC na DAC tunawashukuru sana, TACAIDS na wadau wote
waliosaidia kufanikisha kwa uchaguzi huo katika konga mpya ya Kigamboni.
Mapambano dhidi ya VVU
na UKIMWI ni mapambano endelevu, kila mmoja kwa nafasi yake hana budi
kuhakikisha kuwa anapigana kwa nguvu zote kuhakikisha tunatokomeza janga hili
la UKIMWI.
Post a Comment