Baraza la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA) mnamo Tarehe 22/7/2017
tulikuwa na uchaguzi wa viongozi katika Konga mpya ya Ubungo, uchaguzi huo
ulifanyika katika ofisi ya manispaa ya Ubungo, ambapo wajumbe 39 kutoka katika
vikundi vya WAVIU na Mitandao ya WAVIU, vilivyopo katika kata za wilaya ya
ubungo, Mratibu wa UKIMWI wa Manispaa, Afisa Maendeleo ya Jamii na Vijana, Ofisi
ya Mkurugenzi wa Manispaa, Mwenyekiti wa kamati ya UKIMWI halmashauri ya
manispaa ya Ubungo, Makatibu kutoka Konga za Temeke na Ilala, Mwenyekiti konga
ya Kinondoni, Mwakilishi kutoka mfuko wa kudhibiti UKIMWI (ATF), Ofisi ya NACOPHA Kanda ya Dar es
Salaam, na Mratibu wa kanda toka JSI.
Uchaguzi huu
uliratibiwa na kufadhiliwa na Shirika la JSI kupitia mradi wa CHSSP
unaofadhiliwa na USAID. Katika uchaguzi huo uliochukua takriban masaa nane
ulifanikiwa na viongozi wafuatao waliweza kuchaguliwa:-
1. Kyara Lweno-
Mwenyekiti
2.Reinfrida Chitokota- Makamu
Mwenyekiti
3. Jacqueline Alois- Katibu
4.Juliana P. Jaribu- Mweka
hazina
5.Salum Kondo- Mjumbe
mwakilishi wa Wanaume
6.Enos Tossye- Mjumbe
mwakilishi wa Wanaume
7.Neema Duma- Mjumbe
mwakilishi wa Wanawake
8.Salama Ally- Mjumbe
mwakilishi wa Wanawake
9.Lucian Elias - Mjumbe
mwakilishi wa Vijana wa Kiume
10. Anna Sajilo- Mjumbe
mwakilishi wa Vijana wa Kike
Wawakilishi katika
kamati ya UKIMWI ya Manispaa (CMAC)
1. Rogers Kaitila
(Mwanaume)
2 .Mary Kuzenza
(Mwanamke)
NACOPHA inatoa pongezi
kwa viongozi hao waliochaguliwa na kuwataka watekeleze wajibu wao kufuatana na
sheria ya baraza inavyowataka wafanye. Hivi sasa Baraza lina konga zipatazo 154. Baraza linatowa shukrani kwa JSI kupitia
mradi wa CHSSP kwa kufanya kazi kwa Karibu na Baraza kwa kuhakikisha malengo ya
pamoja ya kufikia 90%,90%,90% yanafikiwa. Bira kusahau Serikali kupitia kwa
viongozi wa wilaya, CHAC na DAC tunawashukuru sana, TACAIDS na wadau wote
waliosaidia kufanikisha kwa uchaguzi huo katika konga mpya ya Ubungo.
Mapambano dhidi ya VVU
na UKIMWI ni mapambano endelevu, kila mmoja kwa nafasi yake hana budi
kuhakikisha kuwa anapigana kwa nguvu zote kuhakikisha tunatokomeza janga hili
la UKIMWI.
Post a Comment