Mbio
za Mwenge wa Uhuru tangia mwanzo zimekuwa kichocheo kikubwa katika kuhamasisha
Maendeleo, uzalendo, Umoja, Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya Taifa
letu. Mwaka huu utakuwa mwaka wa 24 tangu mbio za Mwenge wa Uhuru zirejeshwe
chini ya utaratibu wa usimamizi wa serikali. Lengo ni kutimiza adhma iliyowekwa
na waasisi wa Taifa hili wakati wa kuanzisha Mbio za Mwenge kama kichocheo
kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo, uzalendo, Umoja, Mshikamano na kudumisha
Amani ndani na nje ya Taifa letu.
Mnamo tarehe 27/5/2017, ilikuwa ni fursa ya kuzinduliwa kwa ofisi ya Konga ya Temeke, iliyopo katika kata wa Mwembeyanga. Ofisi hiyo ilizinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mh. Amour Hamud Amour.
Katika Uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Baraza la
Watu Wanaoishi na VVU Tanzania Ndg. Justine Mwinuka ambaye
pia alishiriki katika uzinduzi wa ofisi ya Konga ya Temeke ,
aliishukuru Hamashauri ya Wilaya ya Temeke kwa niaba ya Baraza la taifa la watu
waishio na VVU kwa kutupatia Ofisi hiyo.
Mwenyekiti wa Baraza alipongeza uongozi
wa Konga ya Temeke jinsi walivyowaunganisha WAVIU wa Temeke na kuwa na
mshikamano na kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili
WAVIU.
Akitembelea banda la WAVIU kiongozi wa mbio
za mwenge Mh. Amour Hamud Amour akiambatana na Mwenyekiti wa Baraza
la WAVIU Tanzania Ndugu Justine Mwinuka walishuhudia kazi mbalimbali
zinazofanywa na WAVIU za ujasiriamali ili kujiongezea kipato kwa kupatiwa
mitaji kutoka Halmashauri, na Kupitia miradi Mbalimbali inayotolewa na wadau
mbalimbali kwenye shughuli za mwitikio wa UKIMWI.Pia walipata fursa ya kuuliza
maswali na kuweza kujibiwa kwa ufasaha na waliweza kuwatia moyo ili kuhakikisha
wanapambana kufikia 90-90-90
ifikapo 2020
Aidha Mwenyekiti wa Konga ya Temeke Ndugu
Peter Kisima Kwa niaba ya kamati tendaji
ya Konga alitoa shukrani za dhati kwa Halmashauri ya Temeke kwa kushirikiana na
Uongozi wa NACOPHA kupitia Mradi wa Sauti Yetu kwa kuweza kufanikisha upatikanaji wa ofisi ya Konga ya Temeke.
Mkoa
wa Dar es salaam ulipokea Mwenge wa Uhuru siku ya tarehe 25/05/2017 saa kutoka
Mkoa wa Lindi katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya
Tuangoma na kukabidhiwa katika wilaya ya Temeke. Mwenge wa Uhuru utamaliza mbio zake hapa mkoani Dar es
salaam siku ya tarehe 31/05/2017 na kukabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Pwani
siku ya tarehe 01/06/2017 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere
Terminal 1 kwa ajiri ya kwenda Mafia Mkoani Pwani.
Post a Comment