Tarehe 13/2/2017 kulifanyika kikao kati ya uongozi
wa Konga temeke pamoja na ugeni kutoka UNAIDS. Mgeni toka UNAIDS Bi. Maria
Engel mshauri mkuu wa miradi ya UNAIDS hapa nchini akifuatanana Afisa mipango wa
NACOPHA ndg. Richard Muko, na Bi. Victoria Habuya ambaye ni afisa Ufuatiliaji
na tathimini katika mradi wa SAUTI YETU.
Wageni hawa walikutana na wajumbe wa timu ya
Uratibu na mawakili tiba wa konga ya Temeke kwa lengo la kutathmini jinsi konga
za NACOPHA zitakavyoweza kutekeleza miradi ya kijamii ya kupambana na Saratani
ya Shingo ya Kizazi. Pia wakakielezea kikao kwamba kutakuwa na mradi wa
kupambana na shingo ya kizazi utakaofadhiliwa na shirika la Pink Ribbon Red
Ribbon (PRRR) utakao tekelezwa kwa
ushirikiano kati ya NACOPHA na Tanzania Network of Women Living with HIV and
AIDS (TNW+) katika maeneo ya Geita, Njombe, Tanga, Morogoro, Mara na Songwe.

Baada ya majadiliano wajumbe walikubaliana kuwa
njia pekee ni kutoa elimu sahihi juu ya Saratani ya shingo ya kizazi, kampeni
ya upimaji wa mara kwa mara kwa WAVIU na kuunda timu itakayopewa mafuzo ili nao
waweze kuendeleza elimu hii kwa WAVIU wengine (TOT).
Ili miradi kama hii iweze kufikia walengwa inabidi
mikutano na viongozi wa Serikali ya mtaa iandaliwe, pawe na kampeni za
matangazo pia pawe na vipeperushi katika kuhamasisha watu kupima. Aidha
tulikubaliana muda wa upimaji katika vituo vya afya kila siku uongezeke na uwe
endelevu kwa watu wote mchanganyiko.
Story na BAITAN JAPHEES. Katibu Mkuu Konga Temeke
Story na BAITAN JAPHEES. Katibu Mkuu Konga Temeke
Post a Comment