·
Katika kuadhimisha miaka 55 ya
Uhuru wa Tanzania, Baraza la watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA)
linampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe
Magufuli pamoja na Serikali yake katika kuendeleza jitihada za kudumisha Hekima, Umoja na Amani
tulioachiwa na Muasisi wetu Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
·
NACOPHA ina tambua jitihada
zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Rais Dkt. John
Joseph Pombe Magufuli katika shughuli za mwitikio wa UKIMWI kwa lengo la
kufikia mkakati wa kimataifa wa kuhakikisha azma ya kufikia sifuri tatu yaani:
Sifuri maambukizi mapya ya VVU, Sifuri Vifo vitokanavyo na UKIMWI pamoja na
Sifuri unyanyapaa na ubaguzi.
·
NACOPHA inaendeleza
jitihada zake katika kupambana na Virusi vya UKIMWI pamoja na Ubaguzi na
Unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na kuhakikisha kuna
uimarishwaji , udhibiti na ugawaji dawa za ARV,kuhamasisha upimaji wa Virusi
vya Ukimwi, kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Kuhamasisha elimu ya jinsia, Kutoa elimu ya afya ya uzazi kuboresha upatikanaji
kondom za kike, utoaji damu salama kulingana na vigezo vya shirika la afya
duniani. Kuendelea kuelimisha njia za kujikinga na maambukizo pamoja na kutoa
elimu kuhusu mila na tabia hatarishi zinazochangia ongezeko la maambukizo.
·
Tunaimani, Upendo na Matumaini
kwa taifa letu la Tanzania, sote ni Watanzania na bila kubagua hali zetu za
maambukizo tunamchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania.
·
Tanzania bila UKIMWI
Inawezekana.
Post a Comment