T arehe 1 Desemba ya kila mwaka
huwa ni siku ya UKIMWI duniani, Nchi mbalimbali huadhimisha siku hiyo kwa ajili
ya kuwakumbuka waliofariki kwa ugonjwa wa UKIMWI pamoja na kukumbashana
kuendeleza mapambano dhini ya ugonjwa huu hatari ambao hadi hivi sasa hakuna
tiba wala kinga iliyogundulika.
Mwenyekiti wa Baraza pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria katika viwanja vya mwananyamara kwa kopa katika kuadhimisha siku ya ukimwi duniani "Hands up for #HIV prevention" |
Pamoja na hayo katika siku hii, watu
wote hukumbushwa kipima na kuzilinda afya zao bila kusahau kuwajali wale wanaoishi
na maambukizo ya Virusi vya UKIMWI. Elimu madhubuti hutolewa jinsi ya kuishi
ukiwa tayari Una maambukizo ya VVU kwani ukigundulika kuwa unamaambukizo ya VVU
unatakiwa kuanza/ kuanzishiwa tiba mara moja na kusisitizwa kuto acha kunywa
dawa za ARV kwa ajili ya kuvubaza na kupunguza makali ya VVU ili usifikie hatua
ya UKIMWI ambayo ni hatari Zaidi.
Kuwa na Virusi vya UKIMWI siyo
mwisho wa maisha kwani mtu aishiye na maambukizo ya VVU kwa kutumia dawa za ARV
ataweza kuishi maisha marefu, kuwa na nguvu ambazo zitamsaidia kujikimu kimaisha
kwa kuendelea kujishughulisha kwani mwili unakuwa na nguvu hivyo mtu huweza
kuishi maisha marefu.
Katika jamii zetu kumekuwa na
changamoto nyingi na mitazamo tofauti dhidi ya watu wanaoishi na VVU.
Watu
wanadhani kuwa ukiwa karibu na mtu anaeishi na VVU basi na wewe utaweza kupata
maambukizo hayo. Elimu madhubuti bado inahitajika katika jamii zetu, ili
kupinga unyanyapaa na matendo maovu wanayofanyiwa watu wanaoishi na VVU.
UKIMWI ni ugonjwa kama yalivyo
magonjwa mengine ya Kansa, Presha, Malaria, Kipindupindu, n.k ambayo yasipotibiwa
au kupewa angalizo la juu hupelekea kifo.
UKIMWI husambazwa kwa damu ya mtu
mwenye Maambukizo kukutana na damu ya mtu asiyekuwa na maambukizo. Damu hiyo
huweza kukutana kipindi watu wanapofanya ngono bila kutumia kinga (kondom),
kushirikiana kutumia vifaa vyenye ncha kali na mtu mwenye VVU, mama mwenye VVU
kwenda kwa mtoto (kipindi cha kujifungua au kumnyonyesha mtoto), pamoja na
kuhamishiwa damu iliyokuwa na VVU. Hizo ndio njia kuu zinazoweza kusababisha
maambukizo ya VVU toka kwa mtu mwenye VVU kwenda kwa mwingine.
Katika Wilaya ya Kinondoni, Konga
ya Kinondoni iliyoanzishwa na BARAZA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI
(NACOPHA) iliadhimisha siku hiyo ya UKIMWI duniani katika viwanja vya
Mwananyamala kwa Kutoa Elimu kwa jamii, Kupima na kugawa Kondom bure.
Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu
“Tuungane
Kutokomeza Maambukizo Mapya ya Virusi vya UKIMWI” yalihudhuliwa na
Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) Ndugu
Justine Mwinuka ambaye ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi wa Maadhimisho hayo pia wadau
mbalimbali wa UKIMWI katika Mkoa wa Dar es Salaam na Wananchi kwa pamoja
walikuwepo kuadhimisha siku hiyo.
Mwenyekiti wa Baraza aliwataka
wananchi kuondokana na dhana Potofu juu ya Ugonjwa wa UKIMWI na Kuacha vitendo
viovu vya unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na VVU. Pia alisistiza matumizi
sahihi ya Dawa kwa wanaoishi na VVU, kutokuacha dawa kutokana na masuala ya
Imani potofu pamoja na lugha rafiki kwa wahudumu wanaowahudumia watu wanaoishi
na VVU katika vituo vya kuchukulia dawa.
Vijana waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani wakiwasha mishumaa kama ishara ya kuwakumbuka wale wote waliofariki kwa ugonjwa wa UKIMWI . |
Maadhisho hayo yaliambatana na burudani mbalimbali zilizokuwa na elimu ya UKIMWI kutoka katika vikundi vya Sanaa. Kulikuwa na ngoma za asili, sarakasi, nyimbo, pamoja na mchezo wa asili wa kucheza na nyoka.
Ngoma ya Asili ilivyokuwa ikiburudisha katika kuazimisha siku ya UKIMWI duniani |
Post a Comment