Serikali imesema asilimia 55 hadi 60 ya fedha zitakazopatikana katika Mfuko wa Udhamini wa Ukimwi uliozinduliwa leo zitatumika kwa ajili ya dawa za ARV na magonjwa nyemelezi ya zinaa.

Meneja mpango wa taifa wa kudhibiti Ukimwi kutoka Wizara ya Afya - Dkt. Angela Ramadhani.

Hayo yamesemwa na Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Angela Ramadhani.
Amesema pamoja na matumizi hayo ya fedha watahakikisha upatikanaji wa dawa ni wa kuridhisha nchini hasa kwa vituo vya afya vilivyopo maeneo yasiyofikiwa na huduma za afya kwa usahihi.
Amesema watendaji wanaokiuka masharti ya serikali kwa kuwanyima wagonjwa dawa ofisi yake haitasita kuwachukulia hatua.