·         Tujikumbushe
·         Historia ya Siku ya Wanawake:

·        
Siku ya Wanawake ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1900 kwa kupitia wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani walioandamana kupinga mazingira duni ya kazi zao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira. Kutokana na hali hiyo, nchi ya Marekani ilikubali kuwa na siku ya maadhimisho ya kitaifa ili kutafakari masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wa wanawake.

·         Baadaye Umoja wa Mataifa ulipaoanzishwa mwaka 1945, ilipofika tarehe 8 Machi iliridhiwa iwe Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani. Uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa ulitokana na kukubali kwake kwamba masuala ya haki, maendeleo na usawa wa wanawake yalihitaji msukumo maalumu na wa pekee.
·         Madhumuni ya kuadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ni kuwezesha jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali za Kimataifa/ kikanda na kitaifa zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia na wanawake katika kuhakikisha haki za wanawake kiuchumi, kijamii, na kisiasa zinapatikana na zinalidwa.
·          
·         Aidha, kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ni kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutambua na kuthamini uwezo na mchango mkubwa wa wanawake katika kuleta maendeleo, kuelezea jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali na wadau wengine katika kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kijamii ili waweze kushiriki kikamilifu kujiletea maendeleo yao, familia zao na Taifa kwa ujumla.
·         Tanzania ilianza kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka 1996, maadhimisho yamekuwa yakiandaliwa Kitaifa na katika ngazi ya mkoa.

     Hivyo maadhimisho ya mwaka huu 2017 yanasisitiza Kaulimbiu ya kitaifa ambayo ni; “TANZANIA YA VIWANDA: WANAWAKE NI MSINGI WA MABADILIKO YA KIUCHUMI”.