Wito huo umetolewa na Mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Mbeya Bwana EDWIN MWELEKA wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya utambulisho na kuandaa mpango wa utekelezaji wa mradi wa SAUTI YETU unaofadhiliwa na shirika la misaada ya maendeleo la kimataifa la Marekani (USAID) na kutekelezwa Baraza la Taifa la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA).

Warsha hiyo imefanyika Mkoani Mbeya na Kujumuisha waratibu wa UKIMWI wa Halmashauri, Wenyeviti, Makatibu wa konga  wakiwakilisha konga ambao ndio wanufaikaji wakuu na watekelezaji wa mradi wa SAUTI YETU kutoka katika Halmashauri 16  pamoja na Waratibu wa TACAIDS kutoka mkoa wa Njombe, Iringa na Mbeya.


Bwana Edwin amesema anaamini kama mradi wa SAUTI YETU utatekelezwa vyema basi hapatakuwa maambukizi mapya katika jamii. “Tutaongeza idadi ya watu waliopima na kutambua hali zao za maambukizo ya VVU, kuwa na idadi kubwa ya watu waliojua hali zao, kuanza tiba na kuendelea kubaki katika tiba na mwisho tutaweza kuboresha afya na kupunguza wingi wa virusi ndani ya miili yetu”