Hayo yamesemwa
na mratibu wa TACAIDS Mkoa wa MWANZA Bwana Geofrey Chambuko, katika
ufunguzi wa warsha shirikishi kwa ajili ya utambulisho na kuandaa mpango wa utekelezaji
wa mradi wa SAUTI YETU.
UKIMWI wa Halmashauri, wenyeviti na
makatibu wa Konga kutoka katika Halmashauri 19, ambao ndio wanufaika wakuu na
watekelezai wa mradi wa SAUTI YETU unaosimamiwa na Baraza la Taifa la watu
wanaoishi na VVU (NACOPHA), kwa ufadhili wa Watu wa Marekani (USAID).
Katika hotuba yake mgeni rasmi Bwana
Chambuko amesisitiza WAVIU kushiriki kikamilifu kama inavyoelezea Sera ya Taifa ya UKIMWI,kuwa ni wajibu na jukumu kwa jamii yetu watanzania, na mtu mmoja mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha kuwa wanazuia na kudhibiti
maambukizi ya UKIMWI.
Aidha
Bwana Chambuko ametoa wito kwa washiriki na kusema
“mradi huu uwe chachu ya mapambano dhidi ya UKIMWI katika
halmashauri zetu, naamini endapo tutatekeleza vyema mradi huu basi hapatakuwa
tena na maambukizo mapya katika jamii zetu, tutaongeza idadi ya watu waliopima
na kutambua hali zao za maambukizi ya VVU, kuwa na idadi kubwa ya watu waliojua
hali zao na kuanza tiba na kuendelea kubakia katika tiba na mwisho tutaweza
kuboresha afya na kupunguza uwingi wa virusi ndani ya miili yetu. Ningetamani
hili lingeweza kuwekwa kama lengo la kila mmoja wenu aliyepata bahati ya
kuhudhuria mkutano huu”.
Post a Comment