Mnamo tarehe 5 na 6 Februari 2019 chini ya ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNAIDS Ofisi ya NACOPHA Kanda ya Mwanza ilifanya ziara 
ya kimafunzo ya kubadilishana uzoefu juu ya utekeleaji wa shughuli za mwitikio wa
UKIMWI ili kuhakikisha kuwa 90% 90% 90%  zinafikiwa ifikapo 2030.  ( ambapo 90% ya kwanza ni kwa waliopima afya zao watambue hali zao za maambukizi, 90% ya pili ni wanaostahili kupatiwatiba wanapata tiba na kubakia katika tiba na 
90% ya waliopo kwenye tiba wawe na kiwango kidogo cha  Virusi kwenye damu


Katika ziara hiyo Konga za Halmashauri ya Igunga na Biharamuro walikuwa wageni walioitembelea konga ya Muleba. Konga hizo ziliwakilishwa na Wenyeviti wa Konga, Waratibu wa kudhibiti UKIMWI Halmashauri (CHAC ), Mwenyekiti wa kamati ya kuzibiti UKIMWI Halmashauri (CMAC), Mwenyekiti wa kamati za kudhibiti UKIMWI ngazi ya kata (WMAC) na viongozi wawili wa Vikundi wezeshi.
 

Wageni hao toka Igunga na Biharamuro walitembelea na kuona miradi mbalimbali inayotekelezwa na vikundi vya wezeshi vya WAVIU vya Tumaini kutoka Kishanda, Imani kutoka Bunganhuzi na Njuna ya June kutoka Mushabago, 
Wanakikundi wa kikundi cha Imani wakionesha moja ya miradi yao ya ufugaji wa mbuzi
pia walitembelea Vituo vya Tiba na matunzo (CTC - Care and Treatment Center) vilivyopo Buganguzi na kituo cha Afya cha Rushwa.

Wageni wakipata maelezo kutoka kwa Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Buganguzi
Viongozi wa  Biharamuro, Igunga  na Muleba walipendezewa na ziara hiyo ya mafunzo na kubadilishana uzoefu  na kupendekeza kufanyika mara kwa mara. Pia walitoa uzoefu wao kama mapendekezo kwa konga ya Muleba na Vikundi Wezeshi vya Konga hiyo.
 
Pamoja na mapendekezo hayo waliyoyatoa waliwashukuru na kuwasifu Konga na Vikundi Wezeshi vya WAVIU wa Muleba kwa vitu vifuatavyo:-

         Kuratibu na Kusaidia Vikundi vya Wezeshi vinavyoundwa na halmashauri ya Muleba
·        Huduma za ART zinazotolewa katika ngazi ya kituo
Huduma, Ushirikiano na utetezi kwa WAVIU unaotolewa katika zahanati/CTC ya Rushwa na Buganguzi
         WAVIU wengi wa Konga Muleba Virusi vyao vimefubaa kitu kinachowawezesha kujikita zaidi kwenye shughuli za maendeleo ya kiuchumi na Kijamii 
         Msaada unaotolewa na vikundi vya Wezeshi  katika kuwalea watoto yatima  wanaoishi na VVU na wasiokuwa na VVU

Watoto wanaolelewa na kusomeshwa na wanakikundi wa kikundi cha Imani baada ya wazazi wao kufariki
Tushebe Matunda ni mtoto wa miaka minne (4) anaelelewa na wanakikundi wa Tumaini Kishanga baada ya Mzazi wake kufariki siku sita kabla ya kujifungua

Baada ya ziara hii kulifanyika kikao cha majumuisho kwa konga zilizoshiriki Igunga, Muleba na Biharamulo kwa kuangalia nini wamejifunza ,nini wanashauri kifanyiwe kazi na kukubaliana ni kipi wanakwenda kufanyia kazi ambapo moja ya ahadi zilizotolewa ilikuwa
ya mwenyekiti wa Halmashauri ya Igunga bwana Lucas Bugota aliyeahidi kuwa " mimi pamoja na viongizi wa Konga tuliokuja kujifunza tukitoka hapa tutaenda kuandaa mpango kazi kwa ajili ya utekelezaji wa yale yote tuliojifunza tunaomba baada ya miezi mitatu mje igunga kwa ajili ya kuona shughuli zetu  tulizozifanyia maboresho na kujifunza pia"


Mnamo 7 Februari 2019,  NACOPHA ilitoa mrejesho/ mapendekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Muleba, aliyefurahia na kupendezwa na kazi kubwa inayofanywa na  Konga ya WAVIU wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.

Kikao cha mrejesho wa ziara na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba Mhe. Emanuel Sherembi
Mapendekezo yaliyotolewa ni pamoja na Halmashauri zione jinsi gani zitawatumia WAVIU/ Wakili tiba kusaidia kutoa huduma ambazo sio za kitabibu katika vituo vya afya ili kupunguza adha ya upatikanaji wa huduma katika vituo vya tiba na matunzo, Mashirika yanayofanya miradi ya afua za UKIMWI kutumia mfumo rasmi wa konga kufanya kazi na WAVIU tofauti na ilivyo sasa wanawatumia WAVIU bila kupita Konga ,Viongozi wa dini wapewe mafunzo juu ya masuala ya VVU/UKIMWI kwa sababu wengi wao wamekuwa wakiwashawishi WAVIU waache dawa mara baada ya kuombewa. 





Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Biharamuro akikabidhi kiasi cha Shilingi elfu themanini na sita za Kitanzania kwa Mlezi wa Tushebe Matunda baada ya wajumbe waliotembelea kikundi hicho kuguswa na namna kikundi kilivyojitolea kumlea mtoto