Maendeleo
kwenye chanjo ya HIV ndio suala kuu katika mkutano wa dunia wa ukimwi. Mtaalam
wa juu wa ukimwi anasema hawezi kusema lini tiba ya HIV na Ukimwi huwenda
ikaptiakana, lakini anasema amefurahishwa na maendeleo yake.
Wanasayansi
wanaohudhuria mkutano wa 21 wa kimataifa wa Ukimwi mjini Durban Afrika kusini
wanasema bado hakuna chanjo ya kuzuia maambukizo ya HIV na ukimwi.
Mkurugenzi
wa taasisi ya kitaifa ya kimarekani ya afya na magonjwa ya kuambukiza Dr
Anthony Fauci, anasema ni vigumu kutabiri pale chanjo dhidi ya HIV na ukimwi
itapatikana, lakini anasema anamatumaini kuwa wanakaribia kupata tiba.
Japo
hakuna chanjo maalum ambayo imeonyesha matumaini, lakini wanayasayansi
wanaendelea kwa dhati na majaribio ya chanjo HVTN 702. Chanjo hio inayofanyiwa
majaribio ilitokana na majaribio yalofanywa nchini Thailand miaka michache
ilopita na inaonyesha kiwango fulani cha ufanisi. Majaribio ya chanjo hiyo
yanategemewa kuanza huko Afrika kusini na katika baadhi ya mataifa mengine ya
Afrika baadae mwaka huu, lakini Dr. Fauci anasema itachukuwa mda kabla matokeo
kupatikana.
Post a Comment