Mratibu kutoka Baraza
la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Bw. Joseph Muhoja
(kulia) akizungumza na vijana wenye umri chini ya miaka 18 kuhusu namna kijana anavyopaswa kujitambua na maambukizi
ya virusi vya ukimwi leo katika viwanja vya Sabasaba kuelekea kilele cha Mbio
za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu.
Mwezeshaji kutoka
Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Bw. Hamidu Mkwinda
(kushoto) akiwafundisha vijana wenye umri chini ya miaka 18 juu ya maambukizi ya
virusi vya ukimwi na namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi leo
katika viwanja vya Sabasaba kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani
Simiyu.
Baadhi ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 wakifuatilia mada iliyokua ikitolewa na Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi leo katika viwanja vya Sabasaba kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu.
Mratibu kutoka Baraza
la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Bw. Joseph Muhoja katika picha
ya pamoja na vijana walioshiriki mafunzo ya kujitambua, pamoja na namna ya
kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi leo katika viwanja vya Sabasaba
kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu.
Mjumbe kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Bibi.
Happiness Malamala (kulia) akitoa elimu ya namna ya kutumia kinga kuzuia
maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vijana waliotembelea banda la NACOPHA leo
katika viwanja vya Sabasaba kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani
Simiyu.
Mratibu kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi
na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Bw. Joseph Muhoja (waliokaa katikati) akitoa
elimu kwa kijana aliyetembelea banda la NACOPHA leo katika viwanja vya Sabasaba
kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu.
Mwezeshaji kutoka
Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Bw. Hamidu Mkwinda
(kulia) akitoa elimu ya kujitambua na namna ya kujikinga na maambukizi ya
virusi vya ukimwi wakati wa ziara ya wajumbe kutoka NACOPHA walipotembelea
katika kituo cha mabasi cha Somanga leo katika Mkoa wa Simiyu kuelekea kilele
cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Vijana wakifanya
mashindano ya kula biskuti na kunywa soda wakati wa ziara ya wajumbe kutoka
Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) walipotembelea
kituo cha mabasi cha Somanga kutoa elimu ya nanma ya kujitambua na kujikinga na
maambukizi ya virusi vya ukimwi leo Mkoani Simiyu kuelekea kilele cha Mbio za
Mwenge wa Uhuru
Kijana aliyepata mafunzo ya kujitambua na
kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi Bi. Rose Aloni (kushoto)
akisambaza elimu aliyoipata kwa kijana mwenzake wakati wa ziara ya wajumbe kutoka
Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) walipotembelea
kituo cha mabasi cha Somanga kutoa elimu ya nanma ya kujitambua na kujikinga na
maambukizi ya virusi vya ukimwi leo Mkoani Simiyu kuelekea kilele cha Mbio za
Mwenge wa Uhuru.
Baadhi ya vijana na
watoto waliojitokeza kupata elimu ya kujitambua pamoja na namna ya kujikinga na
maambukizi ya virusi vya ukimwi wakati wa ziara ya wajumbe kutoka Baraza la
Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) walipotembelea kituo cha
mabasi cha Somanga kutoa elimu ya nanma ya kujitambua na kujikinga na
maambukizi ya virusi vya ukimwi leo Mkoani Simiyu kuelekea kilele cha Mbio za
Mwenge wa Uhuru.
Picha/Habari na:
Genofeva Matemu
Vijana nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao ili waweze kujitambua na kupata mbinu mbadala zitakazowazesha kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi ili kujenga taifa lililo na afya bora.
Vijana nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao ili waweze kujitambua na kupata mbinu mbadala zitakazowazesha kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi ili kujenga taifa lililo na afya bora.
Hayo yamesemwa
na Mwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi
(NACOPHA) Bw. Hamidu Mkwinda alipokua akizungumza na vijana waliojitokeza kupata elimu ya namna ya kujikinga na
maambukizi ya virusi vya ukimwi wakati wa wiki ya vijana kitaifa na kilele cha
Mbio za Mwenge wa Uhuru leo katika Viwanja vya Sabasaba Mkoani Simiyu.
“Vijana
wanatakiwa kujitambua na kujua haki zao ili wasije wakaangukia katika wimbi la
ulaghai na anasa ambazo zitawapelekea kutokufikia malengo yao na wakati
mwingine kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi bila kutarajia” amesema Bw.
Mkwinda.
Aidha Bibi.
Happiness Malamala kutoka NACOPHA amewataka vijana kutokukata tamaa pale
wanapojitambua kuwa wamepata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwani kuwa na
virusi vya ukimwi sio mwisho wa maisha bali watambue kwamba virusi vya ukimwi
ni kama magonjwa mengine yasiyotibika kama vile kisukari, kansa na presha.
Naye Mratibu
kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Bw.
Joseph Muhoja amesema kuwa NACOPHA inashiriki katika Wiki ya Vijana kuelekea
kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kuhakikisha vijana wanajua haki zao za msingi hususani vijana wa
kike waliopata jukumu la kuwa wazazi katika umri mdogo wajue aina ya ukatili wa
kijinsia na jinsi ya kukabiliana nao.
Bw.
Muhoja amesema kuwa NACOPHA imejipanga kutoa
amasa kwa vijana kuhusu ushauri nasaha
na kupima ili wajue hali yao ya kiafya na jinsi ya kujikinga na kuwakinga wengine,
lakini pia kupitia maonesho haya vijana wanapata elimu ya afya ya uzazi na
makuzi ili vijana waweze kujikinga na mimba zisizotarajiwa au kupata watoto
katika wakati usio sahihi.
Post a Comment