Konga ya Baraza la Taifa la Watu waishio na Virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA) halmashauri  ya wilaya ya Kinondoni imefanya uchaguzi wa viongozi wa konga hiyo mapema tarehe 23 /2/2019 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya kinondoni.

Uchaguzi ulifanyika kwa ufadhili wa watu wa Marekani (USAID) Kupitia Mradi wa CHSSP unaotekelezwa na JSI, ambao moja ya malengo yake ni kuzijengea uwezo Konga katika masuala ya uongozi bora.


Uchaguzi huo ulisimamiwa na Viongozi kutoka halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, Mratibu wa NACOPHA Kanda ya Dar es Salaam, wenyeviti wa kamati ya kudhibiti UKIMWI (CMACs), Mwakilishi wa mratibu wa UKIMWI ngazi ya halmashauri (CHACs) Mwakilishi wa Mratibu wa UKIMWI wilaya upande wa tiba (DACC) pamoja na Mratibu wa Mradi wa CHSSP kutoka JSI.

Wageni waliohudhulia kushuhudia uchaguzi huo ni pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Konga jirani ambazo ni  Temeke, Ilala, Kigamboni na Ubungo.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni pamoja na:
Mwenyekiti - Juma Galaba.                          
makamu-nikokwisa Jeremiah.
Katibu-Suleiman Lweno.
Mwekahazina-Kisa Mbonile.

Viongozi wengine waliochaguliwa ni wajumbe wa Konga, Uwakilishi wa Vijana, Me - Said hamis na Mansue Ramadhani.  Ke- Shan Ally na Catherin Swai , Wawakilishi wa Wazee me- Mtume Mmakasa na Shahaban Bwanga. Ke ni Aisha kupanga na Doto Sanga pamoja na wajumbe wawili watakao wakilisha katika kamati ya kudhibiti UKIMWI ya Wilaya (CMAC) ambao ni Majuto Mwinyihija na Margret   Sinda
 
Baraza kupitia Afisa Mtendaji Mkuu inatoa pongezi kwa viongozi waliochaguliwa na kuwataka watekeleze wajibu wao kufuatana na sheria ya baraza inavyowataka wafanye “Nawapongeza Sana. Viongozi wote karibuni kwenye ofisi yenu tujuane tupange kazi kwa pamoja, msihofu tuko tayari kwa uwajibikaji. Ahsante kwa uongozi uliopita kuwezesha hili pamoja na JSI na ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa pamoja na CHAC. Ahsante Mratibu wa Kanda ya Dar es Salaam kwa kutuwakilisha. Ahasante Viongozi wa Konga zingine kwa kuonyesha mshikamano. Tushikamane sote kwa maslahi na ustawi wa WAVIU wote Tanzania” shukrani za Afisa Mtendaji Mkuu.
 

Hivi sasa Baraza lina konga zipatazo 167. Baraza linatoa shukrani za dhati kwa JSI R&T kupitia mradi wa CHSSP kwa kufanya kazi kwa Karibu na Baraza kwa kuhakikisha malengo ya pamoja ya kufikia 90-90-90 yanafikiwa.