Tarehe 1 Desemba ya kila mwaka huwa ni siku ya UKIMWI duniani, Nchi mbalimbali huadhimisha siku hiyo kwa ajili ya kuwakumbuka waliofariki kwa ugonjwa wa UKIMWI pamoja na kukumbushana kuendeleza mapambano dhini ya ugonjwa huu hatari ambao hadi hivi sasa hakuna tiba wala kinga iliyogundulika.



Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania Bw. Deogratius Rutatwa akizungumza katika kipindi cha KUMEKUCHA kinachorushwa na ITV Tanzania katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani Disemba 1,  2017
Wananchi wakiwa kwenye maandamano wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017
 Maandamano ya Wadau wa UKIMWI wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam mgeni rasmi wa maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.

Kwa mwaka huu wa 2017 maadhimisho haya kitaifa nchini Tanzania yalifanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam ambapo katika kilele cha maadhimisho hayo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan. Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “Changia mfuko wa Udhamini wa UKIMWI okoa maisha” 
maandamano wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017
Pamoja na hayo katika siku hii, watu wote hukumbushwa kipima na kuzilinda afya zao bila kusahau kuwajali wale wanaoishi na maambukizo ya Virusi vya UKIMWI. Elimu madhubuti hutolewa jinsi ya kuishi ukiwa tayari Una maambukizo ya VVU kwani ukigundulika kuwa unamaambukizo ya VVU unatakiwa kuanza/ kuanzishiwa tiba mara moja na kusisitizwa kuto acha kunywa dawa za ARV kwa ajili ya kuvubaza na kupunguza makali ya VVU ili usifikie hatua ya UKIMWI ambayo ni hatari Zaidi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa serikali wakipokea maandamo (hayapo pichani) wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam


Mwenyekiti wa NACOPHA Taifa Bwana Justine Mwinuka akisoma risala iliyoandaliwa kwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani 2017 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam
Kuwa na Virusi vya UKIMWI siyo mwisho wa maisha kwani mtu aishiye na maambukizo ya VVU kwa kutumia dawa za ARV ataweza kuishi maisha marefu, kuwa na nguvu ambazo zitamsaidia kujikimu kimaisha kwa kuendelea kujishughulisha kwani mwili unakuwa na nguvu hivyo mtu huweza kuishi maisha marefu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa Serikali na  Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU (NACOPHA) wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam
Katika jamii zetu kumekuwa na changamoto nyingi na mitazamo tofauti dhidi ya watu wanaoishi na VVU. Watu wanadhani kuwa ukiwa karibu na mtu anaeishi na VVU basi na wewe utaweza kupata maambukizo hayo. Elimu madhubuti bado inahitajika katika jamii zetu, ili kupinga unyanyapaa na matendo maovu wanayofanyiwa watu wanaoishi na VVU.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU Tanzania Ndugu Justine Mwinuka Mwenye suti nyeusi akiwa na baadhi ya wajumbe wa Bodi Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa NACOPHA mwenye kofia katika Kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani Dec 1 2017 

UKIMWI ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine ya Kansa, Presha, Malaria, Kipindupindu, n.k ambayo yasipotibiwa au kupewa angalizo la juu hupelekea kifo.

Wanachi walihudhulia na wakipima shinizo la Damu wakati wa maadhimisho hayo.

UKIMWI husambazwa kwa damu ya mtu mwenye Maambukizo kukutana na damu ya mtu asiyekuwa na maambukizo. Damu hiyo huweza kukutana kipindi watu wanapofanya ngono bila kutumia kinga (kondom), kushirikiana kutumia vifaa vyenye ncha kali na mtu mwenye VVU, mama mwenye VVU kwenda kwa mtoto (kipindi cha kujifungua au kumnyonyesha mtoto), pamoja na kuhamishiwa damu iliyokuwa na VVU. Hizo ndio njia kuu zinazoweza kusababisha maambukizo ya VVU toka kwa mtu mwenye VVU kwenda kwa mwingine.
Mratibu kutoka Baraza la Taifa la WAVIU Tanzania (NACOPHA), Bi Edna Edson akimuelezea  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan huduma wanazotoa za mapambano ya Ukimwi alipotembelea mabanda katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiwa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) alipotembelea banda hilo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.