Baraza la Taifa la Watu waishio na Virusi vya UKIMWI Tanzania limefanya uchaguzi wa viongozi wa Konga mpya ya Kigamboni mapema 18 /7/2017 katika ukumbi wa CCM uliopo katika kata ya Kigamboni wilayani Kigamboni. Uchaguzi huo uliofanywa kwa ufadhili wa watu wa Marekani (USAID) Kupitia Mradi wa CHSSP unaotekelezwa na JSI ambao moja ya malengo yake ni kuzijengea uwezo Konga katika masuala ya uongozi bora.
Wanakonga wa kigamboni wapatao 31 walihudhulia na kufanikiwa kuwachagua viongozi wafuatao
1.       JOSHUA PIMA NYAGANGO - Mwenyekiti wa Konga ya Kigamboni,
2.       MARIA YUSUF - Makamu Mwenyekiti,
3.       AISHA SAIDI BURE -  Katibu
4.       MWANAHAMISI ISIAKA -  Mtunza fedha (Mweka hazina) wa Konga ya Kigamboni.
 
Pia wajumbe wa bodi ya Konga walichaguliwa ambapo:-
1.      SAUDA MIKIDADI amekuwa muwakilishi wa vijana wa kike
2.      PAUL MICHAE NZIJE muwakilishi wa vijana wa kiume.
3.       NICOLAUS SIKA na IBRAHIM ABDURABI MOHAMED wakiwakilisha wajumbe wanaume
4.      HADIJA SHABANI pamoja na HIDAYA MOMBA wakiwakilisha wajumbe wanawake.
 

Ndugu IBRAHIM ABDURABI MOHAMED alichaguliwa kuwa muwakilishi wa Kamati ya UKIMWI ya halmashauri (CMAC) na Katibu wake ni Bi AISHA SAIDI BURE.
Katika uchaguzi huo wadau mbalimbali wa masuala ya VVU na UKIMWI walihudhuria, kulikuwa na wanavikundi toka katoka vikundi vya WAVIU waliotokea katika kata 9 za kigamboni wapatao 31, CHAC, DAC, Mwakilishi toka TACAIDS, Mwakilishi toka Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni, viongozi toka konga ya Temeke na Ilala ambao walikuwepo kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo.
NACOPHA inatoa pongezi kwa viongozi hao waliochaguliwa na kuwataka watekeleze wajibu wao kufuatana na sheria ya baraza inavyowataka wafanye, pia inatowa shukrani kwa JSI kupitia mradi wa CHSSP kwa kufanya kazi kwa Karibu na Baraza kwa kuhakikisha malengo ya pamoja ya kufikia 90%,90%,90% yanafikiwa. 
Bira kusahau Serikali kupitia kwa viongozi wa wilaya, CHAC na DAC tunawashukuru sana, TACAIDS na wadau wote waliosaidia kufanikisha kwa uchaguzi huo katika konga mpya ya Kigamboni.

Mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI ni mapambano endelevu, kila mmoja kwa nafasi yake hana budi kuhakikisha kuwa anapigana kwa nguvu zote kuhakikisha tunatokomeza janga hili la UKIMWI.