Mbio za Mwenge wa Uhuru tangia mwanzo zimekuwa kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo, uzalendo, Umoja, Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya Taifa letu. Mwaka huu utakuwa mwaka wa 24 tangu mbio za Mwenge wa Uhuru zirejeshwe chini ya utaratibu wa usimamizi wa serikali. Lengo ni kutimiza adhma iliyowekwa na waasisi wa Taifa hili wakati wa kuanzisha Mbio za Mwenge kama kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo, uzalendo, Umoja, Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya Taifa letu.

Mnamo tarehe 27/5/2017, ilikuwa ni fursa ya kuzinduliwa kwa ofisi ya Konga ya Temeke, iliyopo katika kata wa Mwembeyanga. Ofisi hiyo ilizinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mh. Amour Hamud Amour.














Katika Uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wanaoishi na VVU Tanzania Ndg. Justine Mwinuka  ambaye pia alishiriki katika uzinduzi wa ofisi  ya Konga ya Temeke , aliishukuru Hamashauri ya Wilaya ya Temeke kwa niaba ya Baraza la taifa la watu waishio na VVU kwa kutupatia Ofisi hiyo.  

Mwenyekiti wa Baraza alipongeza uongozi wa Konga ya Temeke jinsi walivyowaunganisha WAVIU wa Temeke na kuwa na mshikamano na kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili WAVIU.

Akitembelea banda la WAVIU kiongozi wa mbio za mwenge Mh. Amour Hamud Amour akiambatana na Mwenyekiti wa Baraza la WAVIU Tanzania Ndugu Justine Mwinuka walishuhudia kazi mbalimbali zinazofanywa na WAVIU za ujasiriamali ili kujiongezea kipato kwa kupatiwa mitaji kutoka Halmashauri, na Kupitia miradi Mbalimbali inayotolewa na wadau mbalimbali kwenye shughuli za mwitikio wa UKIMWI.Pia walipata fursa ya kuuliza maswali na kuweza kujibiwa kwa ufasaha na waliweza kuwatia moyo ili kuhakikisha wanapambana kufikia 90-90-90 ifikapo 2020

 Aidha Mwenyekiti wa Konga ya Temeke Ndugu Peter Kisima Kwa niaba ya kamati  tendaji ya Konga alitoa shukrani za dhati kwa Halmashauri ya Temeke kwa kushirikiana    na Uongozi wa NACOPHA kupitia Mradi wa Sauti Yetu kwa kuweza kufanikisha    upatikanaji wa ofisi ya Konga ya Temeke.



Mkoa wa Dar es salaam ulipokea Mwenge wa Uhuru siku ya tarehe 25/05/2017 saa kutoka Mkoa wa Lindi katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma na kukabidhiwa katika wilaya ya Temeke. Mwenge wa Uhuru utamaliza mbio zake hapa mkoani Dar es salaam siku ya tarehe 31/05/2017 na kukabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Pwani siku ya tarehe 01/06/2017 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kwa ajiri ya kwenda Mafia Mkoani Pwani.